Wasanii wa muziki wa asili walioshiriki Tamasha la tatu ta Mtemi Milambo mwaka huu lililofanyika Julai 8-10,201 katika viwanja vya Uyui sekondari Tabora na kufunguliwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mhe.Abeid Mwinyimussa wamepata udhamini wa kurekodi nyimbo za muziki wa asili za makabila ya Kisukuma na Kinyamwezi.
Mwanamuziki wa Ngoma za Asili, Ally Mango(kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga(kushoto) wakizungumzia Tamasha hilo leo Katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga(kushoto) na Mwanamuziki wa Ngoma za Asili, Ally Mango(kulia) wakionyesha baadhi ya Majarida yanayowaonyesha wasanii wa Tamasha lililofanyika mwaka jana.Katika Ukumbi wa Idara Habari Maelezo
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga(kushoto) akifafanua jambo kuhusiana na Tamasha la Tatu la Muziki wa Asili kulia ni Mwanamuziki wa Ngoma za Asili, Ally Mango
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions, Amon Mkonga(kulia)Mwanamuziki wa Ngoma za Asili, Ally Mango(wa pili kulia) wakiwa na wajumbe wa Kampuni hiyo George Shija na Ramadhani Mkulakatika picha ya Pamoja.
Mwanamuziki wa Ngoma za Asili Ally Mango
Waandishi wa Habari wakiwa kwenye Mkutano huo
Ally Mango akionysha Jarida la wasanii wenzake lililofanyika mwaka jana
Wandishi wakiwa katika Mkutano huo
Baadhi ya Wandishi wakiwa Kwenye Mkutano huo.(Picha Zote na Shaaban Mpalule).
Wasanii waliofanya vizuri mwaka huu Ali Mango,Asha Kaombwe,Hamis Mpiga,Paulina Muhala,Paul Magadala wataungana na wasanii wengine wa miaka iliyopita na kuunda bendi ya muziki wa asili iitwayo Mwana Milambo ambayo itakuwa inapiga muziki huo katika mahoteli,maharusi na kumbi mbalimbali za burudani.
Nyimbo zitakazorekodiwa ni Kamnyagara kane, Usoga wi kuwa, Kushoke kukaya, kana nabuta, Sensema malunde, Ng,ombe yalala, Wela wa kulya, Nzagamba ya Sukuma na Miaka hamsini ya Uhuru
Lengo kuu ni kuzihifadhi nyimbo mbalimbali zilizotumiwa na wazee wetu wa kale katika vita, kilimo, harusi,na mazishi.
Nyimbo hizi nyingi huimbwa sehemu mbalimbali lakini ni muhimu kuzirekodi kwa ajiri ya faida ya vizazi vya baadae.
Nyimbo hizo zote zitarekodiwa katika studio ya Aegies chini ya muandaaji maarufu Peter John a.k.a Nice P.
Aksanteni kwa kunisikiliza.
Amon Mkoga
Mkurugenzi Mtendaji wa Chief Promotions.
www.chiefpromotions.or.tz
0755 638 004/0655 638 004
No comments:
Post a Comment